Wednesday, 30 October 2013

Biashara unazoweza kufanya kwa mtaji mdogo sana !!,je? unazijua??.Basi ni hizi hapa zisome

Wengi huamini kuwa lazima uwe na fedha ndio uanzishe biashara na ndio sababu yao kuu ya kukaa bila kujishughulisha,Ukweli ni kwamba mtaji ni moja ya kitu muhimu sana katika kuanzisha biashara,lakini kuna aina ya biashara ambazo zinahitaji gharama ndogo sana kuanzisha na kukupelekea kupata faida kubwa sana.Kama mfanyabiashara unaweza kutoka kwa kishindo sana  kwa kuanza ukiwa huna kitu na kufanya kazi kwa juhudi sana ukiwa upande wa huduma(services) na kufanikiwa kutengeneza faida kubwa na kutokea hapo na kuanza kufikiria kuanza kukodi ofisi yako,kuajiri watu wengine nk ,ingawa ni rahisi kutoka ukiwa upande wa huduma  lakini inahitaji ujuzi au weledi Fulani hivi ili uweze fika kilele cha mafanikio hapa simaanishi lazima uwe umesoma chuo kikuu maana ujuzi au utaalamu wa jambo halihusiani na degree ya chuo kikuu.
Unaweza pata ujuzi kwa kuhudhuria semina mbalimbali,workshop mbalimbali,au kufundishwa na mtu wenye ujuzi husika na baada ya kupata ujuzi kuanza fanyia kazi katika maisha yako ya kawaida kila siku na kuwa bora kwa upande huo.
Nimejaribu kuorodhesha aina zaidi ya 14 unaweza anzisha  pasipo kuwa  na mtaji kabisa au mtaji kidogo sana.Hizi ni aina ya biashara ambazo nimezifanya kwa muda sasa na kuona matunda yake na nyingine nimeshuhudia watu wakifanya na kufanikiwa.
Kama  kweli una shauku la kweli kuanza leo biashara soma  kwa umakini sana na kuona je ni wapi pa kuanzia ili uweze timiza lengo lako la maisha:
Zifuatazo ni baadhi ya biashara unazoweza anzisha kwa mtaji mdogo sana au pasipo mtaji kabisa:
i.                    Huduma za kuandika miradi biashara(business plan),kama ilivyo kwa tafiti za uchanganuzi yakinifu(hali halisi ya biashara)wajasiriamali wengi huwa huepuka kufanya kazi hii ngumu ya kuandika mradi biashara(business plan) yao.Ukweli ni kuwa wajasiriamali wengi hawajui hata kuandika business plan katika uwezo wa kuwashawishi wawekezaji kuja kuwekeza na huwa hawawekezi muda wa kutosha kujifunza kwa hilo.Kama unaweza timiza hitaji hili biashara ipo mikononi kwako.
ii.                  Mshauri wa mambo ya biashara:Wewe ni unauzoefu wa ujasiriamali au mmliki wa biashara?Unajua nini kinahitajika ili uanzishe biashara,kujenga biashara,kuingoza biashara na kukua?Sasa unaweza kuanza kazi ya ushauri wa biashara.Unaweza saidia kampuni au biashara mbalimbali kutoka chini ya uvungu na kwa kutoa ushauri na maelekezo muhimu.Unaweza kuwasaidi watu walioajiriwa kuanza kutoka kwenye ajira na kuingia kwa ujasiriamali kwa malipo.
iii.                Huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu.Wewe ni mzuri katika kuandaa vitabu vya uhasibu vya kampuni au biashara mbalimbali?unaweza weka ulingano kwa vitabu kwa vya uhasibu(hili ni jambo huwa na shauku kulipata)? Sasa hamna kitu kinaweza kukuzuia wewe kuanza huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu anza sasa.
iv.                Kutoa huduma ya kuandaa nakuendesha matukio(Event management),kampuni nyingi kila mara huwa na matukio mbalimbali mfano semina,siku ya familia,sherehe mbalimbali mara nyingi kampuni kama kampuni haiwezi kufanikisha kwa ufanisi uandaaji wa matukio haya,na hivi ndivyo ilivyo kutokana na wafanyakazi wao kuwa na majukumu husika tofauti na kuandaa matukio ya kampuni na kuyasimamia,hivyo ili kuwa na ufanisi hapa inabidi kampuni zikodi watu wan je wenye ujuzi wa kuandaa shughuli husika kwa uhakika,wewe kama una ujuzi na uzoefu wa kuandaa  shughuli kama hizo mwanzo mpaka mwisho uwanja ni wako.Mfano kuna matukio kama siku ya familia,semina kwa wafanyakazi,maonyesho ya biashara ndani nan je ya nchi kwa kampuni husika nk
v.                  Kuanzisha tovuti kwa huduma mbalimbali,Kwa afrika watu kunufaika na tovuti ndio kwanza ipo steji za mwanzoni,Unaweza anzisha tovuti na kutoa huduma ya taarifa watu wanatafuta ,baada kuwa mmiminiko wa watu wengi wanaotembelea tovuti yako,unaweza sasa ongea na kampuni kadhaa kuja kutangaza na wewe  na kutengeneza fedha za kutosha.Kama hujui jinsi ya kutengeneza tovuti usijali kuna tovuti za bure kabisa  ambazo zimetengenezwa tayari kinachohitajika ni wewe kujaza fomu zao na ndani ya dakika moja unakuwa  na wewe tovuti yako,na kama unahitaji nunua domain unaweza ikawa moja kwa moja tovuti yako.Tovuti unazoweza ingia na kutengeneza tovuti yako bure ni www.weebly.com,www.webs.com nk au pia unaweza tengeneza blog ikawa ni  unaweka taarifa watu wanatafuta na kisha kutafut wadhamini wa hiyo blog.
vi.                Mshauri wa masoko,Je wewe unaweza nionyesha mimi njia ya gharama ndogo ya kuongeza wateja wangu kuanzia  aslimia 30% -70% au zaidi?kama ndio biashara ipo mikononi mwako.Unaweza jiweka wewe mwenyewe katika ushauri wa masoko  kwa wamiliki biashara ndogo na kati hata kubwa jinsi ya kuteka na kuwavuta wateja na kuongeza mauzo ya bidhaa kwa ada Fulani ,kutokana huduma husika.
vii.              Mtafasiri wa maandiko mbalimbali kwenda lugha ya wazawa;Kampuni nyingi za nje zinazokuja hapa nchini,huwa wanahitaji kutafsiri taarifa zao kwenda lugha ya wazawa,mfano mradi Fulani,tovuti zao,mfano kama ni kampuni ya vitabu mwandishi mmiliki angependa ili auze kwa wazawa inabidi atafasiri kwenda lugha ya wazawa,Pia mfano kuna hata miradi mbalimbali ambayo inatakiwaiangaliwe na wazawa nk.
viii.            Kutafiti fursa mpya za biashara,Nina marafiki wangu ambao walianza kutoa huduma ya kutafi fursa mpya na wanafanya vema kwenye hii biashara.Wanachofanya kutupia jicho kwa mambo yajayo,mwelekeo,mahitaji aua fursa za biashara;na kuandaa mradi/mpango kuhusiana hilo na kuuza hilo wazo kwa makampuni makubwa.Wakati mwingine wanakuja na mawazo ya bidhaa na mawazo ya biashara yenye soko moja kwa moja kubwa la kutosha;na kuuza hayo mawazo kwa makampuni kwa ajili ya kuayaendeleza.Kama kazi hii unaipenda unaweza anza kutoa hudumu kutafiti fursa mpya za biashara
ix.                Kutoa huduma za ku-print,Biashara hii inafahamika sana na wengilakini bado inalipa sana.Unaweza kuanza kutoa huduma ya ku-print business,banner sposters card,viperushi,flyers,catalogues kwa biashara ndogo na za kati.
x.                  Kutoa huduma za kuajiri,Siku hizi  kazi za managementi za rasilimali watu kwa kampuni nyingi hutolewa na tenda kwa kampuni za nje ya kampuni husika kufanya hiyo kazi ili kuongeza ufanisi kwa kampuni husika na hivyo kupelekea kampuni husika kuweka umakini wake wa kutimiza lengo lake mahususi.Kama una uelewa na ujuzi wa kutosha wa kushughulika na  maswala ya rasiliamali watu uwanja ni wako,kwa sasa hapa Tanzania kujisajili kuwa wakala wa kuajiri ni bure unatakiwa uende pale wizara ya ajira na vijana kujisajili.
xi.                Mshauri wa mitandao ya kijamii (social media consultancy),Kwa hii dunia mitandao ya kijamii imechukua asilimia kubwa sana.Je wewe unajua jinsi ya kutengeneza foleni kwa mitandao ya kijamii?Unajua jinsi ya kuboresha na kuelimisha umma juu ya chapa(brand) za makampuni  ndani ya mitandao ya kijamii kama facebook,twitter na linkedin?Basi unaweza kuwa mashauri wa mitandao ya kijamii na kutengeneza fedha  zako.
xii.              Kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni,Je wewe ni mzuri katika kuandika katiba za kampuni?unajua jinsi ya kuchagua jina  sahihi la kampuni?unajua stepu zinazohitajika ili ukamilishe uandikishe jina la biashara?Anza sasa fungua biashara yako ya kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni .
Huduma nyingine unaweza fanya ili kutengeneza fedha:
xiii.            Kutoa huduma za kuandikisha hakimili za bidhaa au huduma yako
xiv.            Huduma za ushauri kwa biashara ndogo
xv.              Kuandika kitabu kizuri  na kukiuza kwa umma.

Friday, 18 October 2013

Je unatamani kuwa mtaalamu katika kitu unachojishughulisha nacho?,Basi Kuwa mtaalamu na ujiinue kiuchumi kwa kusoma hapa kwa makini !!


Si kila
 anayefanya shughuli fulani
 huwa na 
utaalamu nayo,
wengine wanaifanya kwa kuwa tu nafasi ilitokea  ya kuifanya.
Na hautachukua muda
 kumgundua mtu anayefanya kazi zake kwa utaalamu,
 na yule anayebangaiza njaa tu,
kwa jinsi wanavyoenenda na tabia zao.

Mara nyingi
 waajiri na wateja 
hulalamika kuwa anayewafanyia kazi 
 hana utaalamu.
Yawezekana humalizi kazi vizuri, umemcheleweshea au hata kumzungusha kwa muda mrefu bila taarifa sahihi.

Si mara moja tunasikia 
ni jinsi gani tunatakiwa kuwa wataalamu katika 
shughuli tunazofanya.

Kama unataka kupata mafanikio,
 kuchukuliwa kama mtu makini, 
kuonekana una mchango kwa unaofanya nao shuguli zako,
 kuzifanya kitaalamu ndio njia pekee ya kukufikisha huko.

Lakini tujiulize waajiri/wateja wanatafsiri gani juu ya utaalamu?
Wengi wao watakuona mtaalamu ikiwa wewe:

*Unafika eneo la kazi katika muda unaotakiwa;

*Unaifanya kazi uliyopewa vizuri;

*Unamaliza kazi kwa wakati.

Unadhani kuna matukio mengine ambayo unahisi ukiyafanya yatakuonyesha wewe si mtaalamu?

Kuna matukio ukiwa unayafanya yanakutafsiri moja kwa moja kuwa wewe si mtaalamu wa shaghuli unayofanya.
kwa mfano ukiwa:

*Unachelewesha kazi za watu;

*Unahudhuria vikao ukiwa haujajiandaa;

*Unatumia muda mwingi kuongea umbea muda wa kazi;

*Wavunjia heshima wenzako;

*Wasubirisha wateja muda mrefu bila sababu za msingi;

*Unaiba mawazo ya watu wengine kufanyia shughuli zako bila kuwahusisha;

*Vunja ahadi zako mara kwa mara.

Hebu leo tuangalie njia kumi utakazoweza kutumia kuwa mtaalamu katika shughuli yoyote unayofanya:

Jitahidi kufanya shughuli zako kitaalamu na watu waweze kukuamini, 
kukuheshimu, 
na kukuona una uwezo wa kipekee.
Japo
 mazingira ya kila kazi 
yanatofautiana lakini 
linapokuja suala la utaalamu huwa
 na tafsiri moja dunia nzima.

Hebu tuangalie sifa za kuwa mtaalamu ni zipi:

1.UMAHIRI:

Lazima
 uwe mahiri katika kile unachofanya,
ukitumia ujuzi na maarifa 
ya kutosha katika kazi yako 
lazima utaonekana mtaalamu na watu.

2.ZINGATIA MUDA:

Watu watakuwa wanakutegemea wewe 
ufike katika muda unaotakiwa 
ili shughuli ziende na 
umalize kwa wakati.
Sio kuendelea kufanya shughuli zako kwa mazoea tu bila kujali muda,
kwani hakuna anayependa kumuamini na kumpa kazi mtu asiyemaliza kwa wakati.

3.UAMINIFU:

Unatakiwa kuwa 
muwazi wa shughuli zako,
 na wale unaofanya/unaowafanyia kazi nao wajue nini kinachoendelea.
Ukianza kujifanya mjanja mjanja, 
katika shughuli unayofanya 
huku 
huwaweki wazi watu wengine 
hakuna atakayekuona mtaalamu hata kidogo.

4.UADILIFU:

Utaonekana mtaalamu 
ikiwa utakuwa unasimamia kanuni za 
shughuli yako.
Hakuna anayependa kumpa kazi mtu asiyejua kufuata kanuni za kazi yake.

5.HESHIMA:

Kama huna heshima kwa watu wengine 
unaofanya nao 
au unaowafanyia shughuli
 basi hautaonekana 
mtaalamu hata kidogo.

6.ONGEZA UJUZI:
Tafuta ujuzi wa ziada,
usiendelee kung'ang'ania ujuzi ule ule 
kila siku. 
        Toka nje ya yale unayoyafahamu
           ili kupata mengine mapya 
     kuongezea katika yale unayayafahamu 
            ili kuboresha zaidi utendaji.


7.MTAZAMO CHANYA:

Kama wewe
 kila siku unaangalia makosa tu bila 
kuwa na mtazamo chanya juu ya shughuli unayofanya
 kuwa mtaalamu itakuwa ndoto kwako.

8.TOA MSAADA:

Wasaidie wenzako unaofanya nao shughuli
 sio kwa kuwa wewe unafahamu kitu 
fulani basi hutaki 
wenzako wafahamu.
Waonyeshe jinsi ya kufanya kazi vizuri pale unapoweza 
na wasikilize pale wanapokuuliza
 maswali.

9.TENGANISHA MATUKIO:

Usihusishe matukio ya nyumbani au
 mtaani na kazi,
ukiwa katika shughuli zako weka mawazo
 yako yote hapo.
Utakuwa mtu wa ajabu
 kufika eneo la kazi na kuanza kushughulikia masuala ya nyumbani 
huku ukiacha kazi haziendi.

10.KUWA MSIKIVU:

Kila mtu
 ana hitaji la kusikilizwa pale 
anapokuwa na 
jambo la kusema,
Kwa hiyo wape watu nafasi ya kukuelezea 
yale wanayodhani yatasaidia 
katika utendaji wa kazi.

KILA MMOJA WETU ANAPENDA KUPATA MAFANIKIO KATIKA SHUGUHULI ILE ANAYOFANYA,
BASI TUANZE SASA 
KUFANYA KAZI KITAALAMU ILI TUWEZE KUFIKIA YALE TUNAYOYATAKA

Monday, 14 October 2013

Je? Unamaliza pesa zako kwa matumizi mapema?,Basi soma hapa ujikomboe!!

Njia pekee ya kutunza pesa ni
 kupunguza matumizi 
yasiyo ya lazima.
Unachohitaji ni kujua pesa unatumia 
zaidi kwenye nini,
hapo ndipo utakapojua ufanye nini ili kupunguza matumizi.

Kila mara
 weka akilini kuwa yawezekana 
unanunua kitu kwa bei rahisi
 lakini 
jiulize ufanisi wake una umuhimu wowote 
au ni kutimiza wajibu tu.

Tambua mahitaji yako 
halafu 
fanya hesabu za namna ya kutumia unachokipata kwa uangalifu.
Tambua kuwa
 ili kupunguza matumizi kufanikiwe ni lazima ubadilishe mfumo wako wa maisha na namna unavyofikiria.

Zifuatazo ni hatua unaweza kuzitumia kupunguza matumizi:

1.TAMBUA UNATUMIA PESA ZAKO KATIKA NINI ZAIDI

 Kama mpaka sasa hujui pesa 
zako unazitumia 
zaidi kwenye nini zoezi
 hili litakushinda.
Ukiwa hujui pesa yako 
unatumia kwenye nini hasa,
kila mara utakuwa mtu wa kushangaa tu 
kuwa hela yako imepungua.
Na wengine
 wanaweza kuwalaumu watu wao
 wa karibu kuwa wamewachukulia 
kumbe ni yeye mwenyewe ndiye aliyefanya matumizi.

2.EPUKA MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA

Kuna matumizi
 mengine hata wewe unayaona kabisa
 kuwa hayana ulazima 
lakini kwa kuwa 
ushazoea ndio unaona ni 
kitu cha kawaida.
Na hivi ndio
 vitu mbavyo unanunua hapa
 baada ya dakika tano ukimaliza kukitumia ushasahau kama hata ulitumia.

3.WEKA KIPAUMBELE CHA UNUNUZI

Weka mkakati wa muda mfupi
 wa kutunza pesa unayopata kwa ajili ya kununua kitu fulani ndani ya muda uliojiwekea.
 Kama kuna kitu 
unataka kununua ijue bei yake halafu anza mkakati wa kutunza pesa kwa ajili ya kukimiliki.
Hii itakusaidia kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.

4.PUNGUZA MATUMIZI YA SIMU

Mawasiliano 
siku hizi ndio yamekuwa yanaongoza kwa matumizi makubwa ya pesa.
Ukiwa hujui muda gani  wa kupiga,
 na muda gani wa kutuma 
meseji utakuwa 
unajimaliza mwenyewe.
Unaweza ukaweka vipaumbele vya watu wa kuwasiliana nao.
Kama unafanya simu za biashara ni kitu kizuri lakini 
kama ni stori tupu hapo
 lazima ujizuie.
5.TENGENEZA ORODHA YA VITU VYA KUNUNUA

Unapoamua
 kuwa unataka kwenda kununua 
vitu fulani ni lazima uwe na orodha maalumu itakayokuongoza ili 
usitumie zaidi ya uliyopanga.
Usijiroge ukatoka nyumbani kwenda kununua vitu huku hujui nini hasa unaenda kununua na gharama yake ni shilingi ngapi?
Utakuja kujuta wakati ushafikia nyumbani ukiwa huna pesa kabisa.

PESA INAYOTUMIKA TU BILA KUJIONGEZA NI SAWA NA KUJIFILISI MWENYEWE.

ANZA LEO KUTUNZA KIDOGO UNACHOPATA ILI KESHO USIJE KUJILAUMU 
ZITAKAPOKWISHA KABISA.