Thursday, 5 December 2013

Kwa nini masikini anazidi kuwa masikini na tajiri anazidi kuwa tajiri !!

 
Katika hali ya kawaida unaweza ukafikiria kwamba masikini ameumbwa kuwa hiyo alivyo na tajiri nae kaumbwa kuwa tajiri,lakini kiukweli sio hivyo kabisa na wala haifanani kabisa.Kwa hali ya uhalisia ni kwamba maskini anakuwa masikini kutokana na maisha yale ambayo yeye ndo ameamua kuishi na tajiri nae vilevile anakuwa tajiri kutokana na maisha aliyoamua kuishi hivyo.Kwa watu wengi sana wanaweza kushangaa nina maanisha nini?Ila ninachomaanisha ni hivi asilimia kubwa ya masikini wengi ndio wanaoishi maisha makubwa na ya gharama kuliko hata maisha ya matajiri.Huwezi kujilazimisha kufikiria kwamba tajiri amependelewa bila kuchunguza uhalisia wa maisha yenyewe yalivyo kama ifuatavyo kaitka mfano huu hapa chini:

Kwa mfano hebu fikiria mtu anayefanya kazi nzito ya mfano kuchimba mitaro,kuchoma mkaa,kuzibua vyoo,kufukua mashimo na kadharika.Hawa watu ndio wanaoongoza kufanya matumizi makubwa sana tofauti na kipato chao.Hawa watu ndo ambao waliokuwa na nafasi kubwa sana ya kujitambua ugumu wa kazi zao na kujizuia matumizi lakini badala yake ndo wanaoongoza sana kwa matumizi makubwa na ya sio na maaana kabisa zaidi ya yenye starehe kubwa.Hawa ndio wanaoongoza sana kuhonga wasichana na wauza baa.Ndio wanaongoza kuacha chenji madukani bila kudai wakidai kuwa ni ndogo bila kujua kuwa elfu kumi ndani yake ina sarafu za shilingi hamsini na mia moja pamoja na mia mbili.Jamii hii ni ya watu ambao hawana uwezo wa kununua nguo mpya wala kusomesha watoto shule nzuri wala kula chakula kizuri zaidi ya kuishi kwa kubahatisha tu.Kwa mfano wangekuwa wanatambua jinsi ambavyo hela yao inavyopatikana kwa taabu sana wangepunguza sana matumizi yao na wangeweza kuwekeza kwenye biashara ambazo zitawasaidia sana kujiongeza kipato chao na kweza kuwa zaidi ya matajiri !!

No comments:

Post a Comment