1. Usitegemee chanzo kimoja cha mapato, kila upatapo wekeza zaidi ili uwe na chanzo cha pili, cha tatu, etc.
2. Hakikisha unanunua vitu ambavyo unavihitaji tu. Ukinunua vitu
ambavyo huna haja navyo, iko siku utashindwa kununua vile unvyovihitaji.
Tumia kwa busara.
3. Usiweke akiba kinachobaki baada ya kutumia bali tumia kinachobaki baada ya kuweka akiba.
4. Kwenye kuwekeza hela yako kwenye biashara yoyote kuwa makini,
usiingie kichwa kichwa. Maji ya mto hayajaribiwi kwa kuingia na miguu
yako yote miwili. Utasombwa na maji au utazama.
Saturday, 23 November 2013
Friday, 22 November 2013
UMASKINI TANZANIA NI HALALI YETU KUWA NAO?
Mada yetu ya leo inatahusu juu ya umaskini wa nchi yetu Tanzania na
maisha ya wananchi wake.Hivi ushawahi jiuliza kama umaskini wa nchi yetu
Tanzania unatokana na nini na unasababishwa na kitu gani?Kwa haraka
haraka umaskini ni ile hali ya kutoweza kujikizi kwa mahitaji ya vitu
muhimu kama vile Malazi, chakula na maradhi.Kwahiyo ukiweza kumudu vitu
hivyo ndio unaepukana na hali ya kuwa masikini lakini kwa nchi kiujumla
ni kwamba masikini ni ile nchi ambayo wakazi wake wanaishi chini ya dola
moja kwa siku.Nchi nyingi za Africa zinaishi chini ya dola moja lakini
zinakutana na mambo makubwa sana yanayowafanya waishi chini ya dola moja
kama vile vita,njaa,ukame na tofauti za kisiasa zinazosababishwa na
serikali tawala na vyama vya upinzani vinazotokea na kugombea madaraka
na wengine kukataa kutoka madarakani hata kama wameshindwa uchaguzi na
kung'ang'ania madarakani tu kwa nguvu.Vita katika Tanzania havijawahi
kuwepo na wananchi wake wameishazoea kuishi kwa amani sana maana hawajui
kabisa tofauti na nchi zingine lakini bado nchi ni maskini na watu wake
ni maskini pia.Mfano wa nchi maskini zenye vita ni kama hivi katika
picha hapa chini:
Hii picha inaonyesha jinsi ambavyo watu hawawezi kufanyakazi zao kwa hali ya amani kutokana na vita hivyo kwa hivyo wananchi wanakuwa na wasiwasi wa maisha yao badala ya kujiwekeza katika shughuli za kilimo au biashara ambazo zinaweza kuwapatia maisha yao ya kila siku.Lakini hali hii ni tofauti kabisa na huku kwetu Tanzania ambako watanzania tumekuwa maskini tu wakati nchi iko shwari na ina neema ya mvua katika sehemu kubwa sana ya Tanzania mfano katika mikoa mingi mvua ipo tu na tena ya kutosha mpaka huwa ina sababisha mafuriko.Hebu angalia baadhi ya maeneno mazuri yenye rutuba na mvua ya kutosha Tanzania katika picha hiz hapa:
Je ni kweli tuendelee kuilaumu serikali yetu inayoshindwa kutumia rasilimali za nchi yetu kwa maendeleo ya wananchi na kuendelea kuwafaidisha wawekezaji wa kigeni na baadhi ya wananosaini mikataba ya kiraghai?Mimi nafikiri tujikwamuwe wenyewe tu kwakwenda kuwekeza katika maeneo kama haya ingawa mwanzo mgumu tuanze hata kwa hilo jembe la mkono baadae tuna weza kujikwamuwa kwa kununua vifaa vingine tukiwa na fedha ya kutosha kwani hata ukuta wa beijing ulijengwa kwa mikono ya wananchi wa china bila mashine na wakaweza.Cha msingi ni kujipanga tu na tukaweza kujikwamua katika hali tuliyonayo badala kuendelea kulaumu serikali isiyokuwa na masikio ya kusikia wananchi wake.Kulima hakuitaji mtaji mkubwa wala ufugaji wa kuku wakienyeji hauhitaji mtaji mkubwa zaidi ya kuwa na uvumilivu tu katika hilo na baadae tuishi katika maisha mazuri na kuikwamua nchi yetu wenyewe na sio kutegemea wanasiasa walaghai wanaojinufaisha wenyewe tu.
Hii picha inaonyesha jinsi ambavyo watu hawawezi kufanyakazi zao kwa hali ya amani kutokana na vita hivyo kwa hivyo wananchi wanakuwa na wasiwasi wa maisha yao badala ya kujiwekeza katika shughuli za kilimo au biashara ambazo zinaweza kuwapatia maisha yao ya kila siku.Lakini hali hii ni tofauti kabisa na huku kwetu Tanzania ambako watanzania tumekuwa maskini tu wakati nchi iko shwari na ina neema ya mvua katika sehemu kubwa sana ya Tanzania mfano katika mikoa mingi mvua ipo tu na tena ya kutosha mpaka huwa ina sababisha mafuriko.Hebu angalia baadhi ya maeneno mazuri yenye rutuba na mvua ya kutosha Tanzania katika picha hiz hapa:
Je ni kweli tuendelee kuilaumu serikali yetu inayoshindwa kutumia rasilimali za nchi yetu kwa maendeleo ya wananchi na kuendelea kuwafaidisha wawekezaji wa kigeni na baadhi ya wananosaini mikataba ya kiraghai?Mimi nafikiri tujikwamuwe wenyewe tu kwakwenda kuwekeza katika maeneo kama haya ingawa mwanzo mgumu tuanze hata kwa hilo jembe la mkono baadae tuna weza kujikwamuwa kwa kununua vifaa vingine tukiwa na fedha ya kutosha kwani hata ukuta wa beijing ulijengwa kwa mikono ya wananchi wa china bila mashine na wakaweza.Cha msingi ni kujipanga tu na tukaweza kujikwamua katika hali tuliyonayo badala kuendelea kulaumu serikali isiyokuwa na masikio ya kusikia wananchi wake.Kulima hakuitaji mtaji mkubwa wala ufugaji wa kuku wakienyeji hauhitaji mtaji mkubwa zaidi ya kuwa na uvumilivu tu katika hilo na baadae tuishi katika maisha mazuri na kuikwamua nchi yetu wenyewe na sio kutegemea wanasiasa walaghai wanaojinufaisha wenyewe tu.
Wednesday, 20 November 2013
Wakati unausikiliza wimbo huu jipe moyo na ujikubali kuwa unaweza kuwa vile unavyotaka uwe !!
Ukijikubali utajiamini,utakuwa na utayari,uvumilivu pamoja na jitihada.
Kamwe usikate tamaa shika sana ulichonacho.
Monday, 18 November 2013
Dalili zinazoonyesha kuwa kazi ufanyayo ni sahihi kwako ama lah !!
Jiulize,
viatu ulivyovaa ni siazi yako na kama ndio ni aina yako?
Miongoni mwetu tunatumia asilimia 75 ya muda wetu kwa siku katika kazi.
Kwahiyo kuwa katika kazi ambayo haikupi faraja inaweza ikakuletea matatizo katika maisha yako ya kila siku.
Umejaribu njia zote kujitahidi kuendana na hali lakini bado unaona wazi kabisa kwamba kuna kitu kinakosekana.
Ni ukweli usiopingika kuwa kazi yoyote ile kwa upande mwingine kuna kipindi inachosha.
Unachopaswa kujiuliza ni je,
hali hii unayojisikia ni ya muda au ni ya kudumu?
Kama ushawahi kukumbana na hali hiyo au kujiuliza hilo swali basi makala hii inakuhusu.
Sasa utajuaje kama kazi uliyopo sasa ulifanya uamuzi sahihi kuifanya au ulikosea?
Zifuatazo ni dalili ambazo unapaswa kuziangalia ili kufahamu na kutatua fumbo hili:
1.HUNA SHAUKU YA KUPANDA DARAJA:
Kama upo
katika kazi unayoipenda kupanda daraja kwako kitakuwa kipaumbele chako
cha kwanza kwani ndicho kitakuwa kipimo cha utendaji wako.
Hivyo hicho ni kitu utakachokuwa unapenda kikutokee.
Kila mfanyakazi hutegemea baada ya kazi apate ujira wake na kuonyesha uwezo wake katika kazi yake.
Lakini
endapo haujawahi kujisikia hali ya kuonyesha uwezo wako ili kupata
daraja jipya basi ujue hiyo si hali ya kawaida kuiacha kama ilivyo.
2.UNAJIONA UKO PEKE YAKO:
Kuwa mfanyakazi si kwenda eneo la kazi,
kukaa katika meza yako,
kufanya kazi yako na kurudi nyumbani.
Ni
kushirikiana na kila mtu aliye eneo lako la kazi, kuchangamana nao,
kujadiliana masuala ya kazi, na kutumiana katika kujipima uwezo wa kila
mmoja wenu.
ikikosekana hali hii eneo la kazi hupoteza ladha ya kukalika.
Ikiwa umewahi kufanya juhudi za kuanza kuchangamana na kushirikiana na wenzako lakini imeshindikana mpaka leo.
Unapaswa ujiulize ni kwanini hali hiyo inatokea.
Inawezekana wenzako wanapishana kabisa na wewe kuanzia malengo mpaka sifa.
3.KILA WAKATI HUISHI KULALAMIKA
Hakuna kazi inayohakikisha kumfurahisha kila anayeifanya kila wakati.
Na lazima katika mabaya yote unakutana nayo lazima kuna machache mazuri yatakuwepo.
Lakini ukijikuta kila kitu unakilalamikia hakuna zuri unaloliona si kitu cha kukiachia hata kidogo,
lazima kutakuwa na tatizo kwako.
Kaa chini uitafakari kazi yako kisha jaribu kuangalia yapi unayaona zaidi mabaya au mazuri,
na endapo mabaya yakiwa mengi basi hiyo ni dalili tosha kwamba unapaswa utafute ustaarabu mwengine.
4.KIPAUMBELE CHAKO NI PESA TU:
Kama ulikuwa
hujui pesa inaweza kukuridhisha kwa miezi kadhaa lakini ikishaisha
kuridhika kutaegemea zaidi uhusiano wako na kazi unayofanya.
Pesa ni muhimu hilo kila mtu analitambua,
lakini hakutakuwa na thamani hata kidogo kufanya kazi usiyoipenda eti kwa kufuata pesa.
5.HAKUNA JIPYA UNALOJIFUNZA:
Katika kila kazi anayofanya mtu lazima kuna vitu vipya utakuwa unajifunza,
na endapo unataka kuongeza uwezo wako wa kufanya kazi ili kupata uzoefu zaidi hiki pia kitakuwa kipaumbele chako.
Soko la ajira linakuwa siku hadi siku na hivyo hitaji la watu wenye uzoefu wa mambo mengi watakuwa hitaji namba moja.
Kama hauna tabia ya kujifunza vitu vipya katika kazi yako basi upo katika hatari kubwa sana ya kupitwa na wakati.
Haina maana kujisifu umekaa miaka mingi katika kazi yako lakini huna jipya ulilojifunza.
6.HUJIONI KUKUA KATIKA KAZI YAKO:
Katika maisha kukua ni sifa mojawapo katika jambo lolote unalojihusisha nalo.
Hautaweza kuipenda kazi ambayo huoni dalili yoyote ya wewe kukua katika siku zijazo.
Kama kilele unachotaka kufikia hakiko
wazi kwako,
sioni ni jinsi gani utaweka juhudi kukifikia.
Kitu hiki hakitaishia kukunyima raha tu, bali kitachukua pia uwezo wako wa kujiamini.
Utaanza kuvurugikiwa na hasa hali itakuwa mbaya pale utakapo kuwa unakutana na watu ambao wamefanikiwa katika kazi zao.
7.HAUIONEI FAHARI KAZI YAKO:
Hata kwa
kiasi gani ujitahidi kujiambia mwenyewe kuwa kazi unayofanya ni nzuri
lakini hauna uthubutu wa kuitaja mbele ya wenzako.
Hivi itawezekana vipi mtu uone aibu kuielezea kazi yako mbele ya wenzako halafu uwe unaipenda?
8.UNAJIHUSISHA NA VITU VYA OVYO UKIWA KAZINI:
Kama unafanya kazi unayoipenda utakuwa unakwepa sana kukutana na mambo ya ovyo.
Muda mwingi utakuwa unawekeza nguvu yako katika kazi unayofanya na si kujihusisha na vitu visivyohusiana na kazi yako.
Endapo
unapenda zaidi kukatisha kazi unayofanya ili kushabikia kitu cha ovyo
kabisa hiyo ni dalili tosha hiyo kazi ujiulize tena.
9.HAUTUMII UWEZO WAKO:
Kazi nzuri ni ile inayokupa nafasi ya kujitumia uwezo wako kwa kiasi kikubwa.
Kama kazi unayojihusisha nayo haikupi nafasi ya kuonyesha uwezo wako wote basi anza kujitafakari kama ulipo ulipaswa uwepo hapo.
Afadhali ujue wazi kabisa kuwa kazi unayofanya umeizidi sifa kuliko iwe ya kawaida lakini uwezo wako ushindwe kuonekana.
Kazi inapofikia hatua hiyo maana yake nafasi ya wewe kukua kiujuzi itakuwa ndogo.
RAHA YA MAISHA NI KUFURAHIA KITU UNACHOFANYA,
IWE INAKUINGIZIA KIDOGO AU KIKUBWA FURAHA NDIO HUWA KIPAUMBELE.
KUFANIKIWA NI ZAIDI YA KUWA KIPATO KIKUBWA
NA MALI.
ANZA LEO KUTAMBUA KAZI UNAYOIPENDA NA UANZE KUISHI MAISHA YA MAFANIKIO KWA KUUTUMIA UWEZO WAKO KAMILI
Tuesday, 12 November 2013
Fanikiwa kimaisha kwa kuyaweka haya katika matendo !!
Ili
uweze kufanikiwa maishani unatakiwa uwe na mipango ya maisha yako.Mara
nyingi watu wengi wamekuwa ni hodari wa kupanga mipango ya harusi na
mambo mengine madogo madogo lakini wanasahu kupanga mipango ya maisha
yao. Kama huna mipango juu ya maisha yako si rahisi kupata mafanikio.
Kuweka malengo ni mchakato wa kufikiria juu ya maisha yako ya baadaye na
kuyabadili kutoka kwenye hali duni au hali uliyonayo kwa sasa na kuwa
yenye mafanikio. Maisha ni safari ndefu hivyo ni vyema ukajua unakwenda
wapi na utafikaje huko unapotaka kwenda.Kujua malengo yako kutakusaidia
kuwa na muelekeo na kukusanya nguvu zako zote kwenye jambo unalolitaka.
Mara nyingi huwa nawauliza watu swali hili ninapiojadili kuhusu malengo,
Jee kama unasafiri na hujui unakokwenda ukifika kwenye kituo cha magari
ya kubeba abiria utapanda gari la kwenda wapi? Wengi hunijibu kwamba
utapanda gari lolote na kwa sababu hiyo, kwa vile hujui unakokwenda kwa
hakika huwezi kufika huko. Huo ndiyo umuhimu wa kuweka malengo kwani ni
sawa na msafiri anayejua anakokwenda hivyo akifika kituoni atajua apande
gari gani na hakika atafika anakokwenda. Kwa hiyo si swala la ajabu
kuona watu wengi wakihangaika kutafuta mafanikio bila kuchoka lakini
hawafanikiwi kwa sababu ya kutojua siri hii.
Kutokuwa na
malengo kumewafanya watu kufanya shughuli nyingi kwa wakati mmoja na
vilevile kuziacha baada ya kuona kwamba ni ngumu.Watu hawa hufanya hivyo
kwa kushawishiwa au kwa kuiga baada ya kuona wengine wakifanya biashara
ya aina fulani. Ndiyo maana mtu mmoja akianzisha duka mtaani basi watu
wengine nao wanaanzisha duka na hivyo unakuta maduka mengi katika mtaa
huo mpaka mengine yanakosa wateja.Mimi mwenyewe nimewahi kukumbwa na
tatizo hili, nimefanya biashara nyingi sana, nimewahi kufanya biashara
ya mtandao kuuza bidhaa za makampuni kadhaa, ukandarasi, vyuma chakavu
na kutengeneza chaki. Baada ya kutafuta ushauri nilifundishwa namna ya
kujiwekea malengo ndipo nikaamua kutoa huduma ya ushauri wa biashara.
Kwa sasa hivi kwa vile ninajua ninachokitaka na nimekwisha jiwekea
malengo yangu siwezi kuyumbishwa na kujishughulisha na biashara
nyingine.
Upangaji wa mipango na kuweka malengo hufanywa na
Wafanyabiashara wakubwa, wanamichezo maarufu na wasanii maarufu.
Utaratibu huu huwasaidia kuwapa muelekeo na malengo ya muda mfupi yaani
mwaka mmoja, muda wa kati yaani miaka mitatu hadi mitano na na muda
mrefu yaani miaka kumi na kuendelea. Pia huwasaidia kukusanya nguvu na
maarifa ili kufikia malengo yao kwa urahisi. Malengo huanzia kwa kuwa na
picha kubwa ya hali halisi unayoitaka kwa kujiuliza ni nini
unachokitaka maishani mwako? Na kisha huvunjwa vunjwa kidogo kidogo .
Maisha ya binadamu yamegawanyika klatika sehemu mbali mbali kama vile
kiuchumi kiafya kisaikolojia na kiafya. Kwa mfano,mafanikio ya ya
mwanafunzi hupimwa kwa maksi zake anazopata darasani lakini kiuchumi ni
jinsi alivyo na pesa nyingi benki pamoja na vitegauchumi alivyonavyo
pamoja na shughuli anayoifanya ambayo inamuingizia kipato. Mambo mengine
ni mahusiano mazuri aliyonayo kwenye jamii na familia yake. Pia bila
kusahau afya yake, kwani hakuna utajiri mkubwa kwa binadamu kuliko afya
yake.
Mambo muhimu ya kujiuliza katika kupanga malengo ni yafuatayo;
Jee unataka kufanya kazi au shughuli gani maishani mwako? Jee
ungependa kupata fedha kiasi gani kutokana na shuguli unayotaka
kuifanya? Jee maarifa/elimu ipi ambayo ungependa kuipata ili kuweza
kukusaidia kufikia malengo yako? Mtazamo gani au ni mabadiliko yapi ya
tabia unayotakiwa kuyafanya ili ufikie malengo yako? Tafakari mambo haya
. Wataalamu wa maswala ya biashara wanashauri ufanye biashara ambayo
inaendana na kipaji au elimu yako, kwani kwa kufanya hivyo utapunguza
muda wa kujifunza mambo mapya. Mara nyingi kuamua ufanye biashara gani
ni suala gumu na mimi nimekuwa nikikutana na watu wakiwa na mtaji lakini
hawajui wafanye biashara gani.
Baada ya kupanga mipango yako
kama nilivyokueleza hapo juu unatakiwa kuanza utekelezaji mara moja. Ni
vyema kila mwaka unapoanza uwe na mipango pamoja na malengo ya mwaka huo
na inapofika mwisho wa mwaka unaangalia malengo yapi uliyoyatekeleza na
yapi hukuyatekeleza. Pia ujiulize sababu zilizosababisha usitekeleze
malengo hayo. Yale mambo/ malengo ambayo hukuyatekeleza mwaka uliopita
unapaswa kuyatekeleza mwaka unaofuata. Katika utekelezaji si mambo yote
unaweza kuyafanya kwa mara moja unaweza kuyapangia mipango kwa mfano
kila siku unaweza kuorodhesha mambo utakayofanya kesho yake kuanzia saa
12 asubuhi saa mpaka saa 12 jioni jambo linaloshindikana leo unalipeleka
kesho. Vivyo hivyo unaweza kupanga mambo utakayoyatekeleza ndani ya
wiki moja na ndani ya mwezi mmoja.
Mwongozo wa namna ya kuweka malengo;
Malengo yaelezewe kwa njia chanya mfano tumia neno ninataka kuwa tajiri
badala ya kuwa ninataka kupambana na umasikini. Unatakiwa kutaja ni
kiasi gani cha pesa uunachokitaka na pamoja na muda gani/lini unataka
upate pesa hizo. Unakiwa uweke vipaumbele kutokana na uzito wa malengo
yako ili ujue unaanza na jambo lipi na kumalizia na jambo lipi. Malengo
yako lazima yaandikwe na ili yasuisahaulike pia unapaswa kuyasoma mara
kwa mara ili usiyasahau. Njia nyingine ya kukusaidia kukukumbusha kuhusu
malengo yako ni kwa kutumia picha. Unaweza kukata picha ya kitu
unachokitaka kwenye magazeti, kwa mfano kama unataka kununua gari ya
aina fulani unaweza kukata picha hiyo na kuibandika sehemu ambayo
unaiona kila mara kama vile kwenye kabati mlango wa chumbani au kwenye
kabati. Unaweza kumweleza mtu unayemwamini kuhusu malengo yako mfano
mkeo mwanao mkubwa au rafiki wa karibu ili aweze kukuhoji kama hutaweza
kufikia malengo hayo. Malengo yako usimwambie kila mtu kwani watu
wengine wanaweza kukufitini na kukukwamisha. Weka malengo ambayo
yanawezekana au yanatekelezeka kufuatana na uwezo wako,kwa mfano usiweke
malengo ambayo yako nje ya uwezo au mazingira yako kama vile katika
biashara, kupanga mipango ambayo haiendani na sheria za nchi mfano
kufanya biashara bila leseni.
Katika kufikia malengo yako
furahia hali kama malengo uliyoyapanga yalikuwa magumu basi jipongeze.
Kama yalikuwa mepesi basi jipangie magumu zaidi. Kama yalikuwa magumu
sana yapunguzie makali. Kushindwa kufikia malengo si tatizo jizoeze
kufanya utaratibu huu kwani unaweza kukusaidia kukufikisha mbali
kimaisha. Ukishindwa kufikia malengo kipindi hiki jaribu kuyapeleka
mbele mwaka ujao. Katika maisha usikate tamaa kwani ukikata tamaa ni
sawa na kuwa mfu. Watu mashuhuri wamethibitisha kwamba unaposhindwa
kufikia malengo hiyo ni kama shule ya maisha jaribu tena na tena mwisho
utafanikiwa.
Jee umekwisha jiwekea malengo katika maisha yako?
Kama hujafanya hivyo nakushauri uanze sasa hivi na utaona jinsi
utakavyoanza kuyapata mafanikio kwa haraka
Saturday, 9 November 2013
Unaweza kujiajiri na wewe !!,fuata hatua hizi !!!
ULISHAWAHI KUFIKIRIA KUJIAJIRI MWENYEWE?
Hili ni swali ambalo litakuwa linakuja kwako kila utakapokuwa unalalamika kukosa kazi uliyoisomea.
Kila mmoja wetu amezaliwa na uwezo huu wa kujiajiri.
Tumezaliwa na shauku, kiu, kufanya mambo ya hatari, uvumbuzi, akili na vitu vingine vingi ambavyo
huonyesha wazi kuwa mtu hawezi kufundishwa ujasiliamali bali uko ndani yake kiasili, kinachohitajika ni yeye
tu kujiweka katika mazingira ya
kuruhusu akili yake kutatua tatizo lililojitokeza sehemu husika.
Hapa ninakuletea mfululizo wa vitu ambavyo unapaswa kufanya ili kuiamsha hamasa ya ujasiliamali ndani yako:
1.TENGENEZA MARAFIKI:
Yeyote anayetaka kuwa mjasiliamali ni lazima atengeneze marafiki wengi wenye mtazamo chanya kama yeye.
Usiwe
na marafiki ambao unatofautiana nao mtazamo, watakuwa wanakukatisha
tamaa kwani kwao hilo wazo wanaona haliwezekani na watakwambia huwezi.
Kauli kama hizo zitakukatisha tamaa na ukizingatia wazo lolote mwanzo huwa gumu na haliwezekani mpaka uanze kulifanyia kazi.
Ndio ule msemo wa ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi unaingia hapa.
2.TENGENEZA LENGO:
Kutengeneza lengo la biashara ni hatua muhimu katika hatua za kuwa mjasiliamali.
Lengo hili uliweke katika maandishi na litakusaidia katika kuwashawishi watu kukusaidia mtaji.
Mara utakapokuwa umeandika lengo la biashara unayotaka kufanya usiweke maandishi hayo kabatini,
anza kuyatafutia njia ya kuwa kitu halisi kutokana na hayo maandishi.
Na pia lengo hili litakusaidia wewe usiyumbe na kutoka katika mstari wa lengo ulilojiwekea na litakuwa ni muongozo wako.
3.JENGA NIDHAMU:
Unapotaka kuwa mjasiliamali ni lazima utengeneze nidhamu yako ya kazi.
Kabla
hujaanza kuingia hatua ya kujiajiri ili uepuke hatari ya kupoteza kila
kitu jiulize kama una nidhamu ya kutosha kuingia katika hiyo shughuli.
Huwezi ukawa mjasiliamali ambaye hauheshimu hata muda wako wa kazi.
4.TAMBUA JAMII INAHITAJI NINI:
Kama
unataka kuwa mjasiliamali ni lazima uwe na uwezo wa kuchemsha akili
yako katika kuyasoma mazingira uliyopo yanahitaji kitu gani na wewe uje
na utatuzi wake.
Lenga eneo moja ambalo unaona kweli lina uhitaji na unaweza ukaja na utatuzi wake.
5.HOJIANA NA WAJASILIAMALI WALIOKUTANGULIA:
Kama unataka kuwa mjasiliamali utapata faida kubwa sana kuzungumza na watu ambao tayari wanafanya ujasiliamali.
Ukiwa na bahati kumpata mwenye moyo wa dhati wa ujasiliamali hatokuficha kitu ili kukusaidia ufikie ndoto yako.
Kwani kiasili mjasiliamali huwa anajitoa kuisadia jamii yake na hana haja ya kuwa mchoyo wa maarifa.
6.TENGENEZA WAZO RAHISI KUTEKELEZEKA:
Kama unataka kuwa mjasiliamali ni vyema ukawa umechagua eneo moja maalumu la kulitafutia ufumbuzi na ambalo
rahisi kutekelezeka.
Na pia kuwa makini hilo jambo unalotaka kulifanyia kazi uwe na uzoefu nalo japo kidogo,
kwani huwezi kutibu ugonjwa usijua hata unakaa wapi.
7.FANYA UTAFITI WA WAZO LAKO:
Ukiwa tayari umeshategeneza utatuzi juu ya jambo fulani jaribu kutafuta maoni kwa watu uliolenga kuwasaidia.
Yawezekana
usiwaeleze kwa kina kuhusu wazo ulilokuja nalo lakini tafuta namna ya
kulijaribu na uone wanatoa maoni gani juu ya utatuzi huo kwa kupitia
huduma za bure na mitandao ya kijamii.
Njia hii ndio itakusaidia kutambua kama wamependa njia yako ya utatuzi au la.
8.FANYA BIDII KULIKO WENGINE:
Hapa lazima utambue kuwa kila mtu anaweza kuwa mjasiliamali,
lakini tofauti huja katika bidii wanayoweka katika shughuli waliyochagua.
Kama umejitolea kuwa mjasiliamali ni lazima ujitoe kufanya kazi kwa bidii kuliko mtu yeyote yule.
9.TAFUTA MSHAURI:
Ukitaka kuwa mjasiliamali ni vizuri ukawa na mtu anayekuongoza kwa mawazo kwani si kila wakati utakuwa unawazo sahihi.
Si kwamba yeye ndio awe anakutengenezea wazo bali anaweza akawa
anapitia wazo lako na kukushauri kama uboreshe au kuna vitu uondoe.
Ikiwa utampata mshauri mzuri itakusaidia kupunguza hatari ya kuumia mapema.
Kuwa makini na mtu utakayemchagua, uwe unamuamini na awe hana ushindani na wewe.
10.HAKIKISHA UNAFURAHIA:
Hapa ni lazima ujue, kama unataka kuwa mjasiliamali mzuri na utakayefanikiwa ni lazima ufanye kitu unachokipenda.
Unapokuwa unafanya kitu unachokipenda unajitengenezea mazingira ya kuwa na furaha muda mwingi.
11.JIUNGE NA WAJASILIAMALI:
Ikiwa unataka kuwa mjasiliamali ni muhimu kutafuta eneo ambalo wajasiliamali wengi wanakutana kujadiliana.
Katika mazingira kama haya utakuwa kama yai linaloatamiwa na kuku ili lije kutoa kifaranga.
Wengi wao huwa wamepitia magumu kufika walipofika na hivyo wakiwa wanasimulia habari zao watakufanya ujiamini.
12.KUWA NA MAONO:
Kama
unataka kuwa mjasiliamali ni lazima uandike maono yako ya unatarajia
kuwa wapi katika shughuli unayotaka kufanya siku zinazokuja.
13.JITANGAZE:
Kama unataka kuwa mjasiliamali utakayefanikiwa ni lazima ujitangaze watu wakufahamu wewe ni nani na unafanya shughuli gani.
Siku zote mjasiliamali anauza jina na si kitu kingine.
Watu wanapokuamini unawafanya waamini kila kitu kinachokuja kwa jina lako.
14.HUDHURIA SEMINA NA MAKONGAMANO:
Wewe
kama unataka kuwa mjasiliamali ni lazima utenge muda wako kuhudhuria
semina mbali mbali, zinazohusiana na shughuli unazotaka kuja kufanya.
Unapohudhuria
maeneo kama hayo itakusaidia kutengeneza mtandao na watu wengine na
hata kukutana na watu wanaoweza kukusaidia kufika unapotaka.
15.FANYIA KAZI HATARI UNAYOIFAHAMU:
Sifa
ya mjasiliamali wa kweli, ni yule asiyeingia kichwa kichwa kutaka
kutatua tatizo pasipo kupiga hesabu za kutosha za hatari iliyopo.
Mjasiliamali,
kweli huwa anachukua hatari za jamii na kujibebesha yeye lakini
anapaswa achukue hatari ambayo hesabu zake anazifahamu.
KWA WALE WOTE WENYE MAWAZO YA KUTAKA KUJIAJIRI, HIZO NI BAADHI YA HATUA AMBAZO UNAWEZA KUZITUMIA KATIKA KUFIKIA NDOTO YAKO.
Sunday, 3 November 2013
Je? unapotaka kusonga mbele matumaini yanapotea??.Basi soma hapa utafanikiwa !!
Maisha yanabadilika; daima yanasonga.
Wewe kubakia hapo ulipo ni chaguo lako mwenyewe.
Na kuna msemo usemao; "Hatima yako inaamuliwa na chaguo lako na si nafasi inayotokea".
Njia ya kufikia mafanikio inaweza kuwa ndefu lakini siku zote huwa pana.
Kama haupendezewi na jinsi maisha yako ya sasa yalivyo,
una chaguo la kubadilisha hali hiyo na mambo yakawa mazuri.
Si lazima ufanye mabadiliko makubwa kwa wakati mmoja bali unaweza ukaanza kwa hatua moja na yenyewe ikazaa nyingine.
Lakini wengi wetu huwa tunakwama wakati wa kufanya maamuzi ya kujikwamua katika hali mbaya ambayo hatuitaki.
Na mambo yafuatayo yanaweza kuwa miongoni mwa sababu zinazotushikilia tusiweze kufikia malengo:
1.KUKWEPA MAJUKUMU
Endapo wewe ni mtu ambaye mambo yanapoenda vibaya unatafuta mtu wa kumlaumu basi ujue unajifunga pingu usiende mbele.
Na hili ndio eneo ambalo kama hautalirekebisha kusonga mbele kwako
itakuwa ngumu.
Kwani uamuzi unaufanya wewe lakini jambo likienda vibaya unatafuta kosa kwa wengine.
Unatakiwa uwe mtu wa kuikubali hali iliyotokea,
jifunze kupitia hiyo na usonge mbele kwa kuboresha utendaji.
2.HOFU IMEKUSHINDA
Kama
unafanya mambo makubwa na kila siku unapigania kutimiza ndoto zako
lazima utakutana na hofu kubwa zitakazokufanya muda mwingine usijiamini.
Lakini hupaswi kuiruhusu hofu ikushinde kwani utakata tamaa mapema sana na mambo hayatoenda,
bali songa mbele kwa kile unachokiamini na hofu ipotezee kwa kuwa jasiri.
3.KUTOUTUMIA UWEZO WAKO
Wewe ndani yako uwe ushajua au bado kuna kitu ambacho ndicho umepewa uwezo wa juu zaidi kukifanya kwa ufanisi.
Lakini ukiwa unafanya jambo fulani ili uwaridhishe watu fulani tu utakuwa unajiingiza shimoni,
kwani mwisho wa siku utakuwa unajishughulisha na vitu ambavyo havitakufanya utumie uwezo wako kamili.
Anza kushughulikia namna ya kutumia uwezo wako halisi kwa kufanya unachokipenda.
4.KUSHIKILIA MAWAZO MABAYA
Kama ndani yako umejijengea tabia ya kukosoa na kutotaka kuangalia upande mzuri wa kitu basi unaangamiza hatua zako.
Usiishi kwa kuweka ndani yako maneno ya watu waliyoongea vibaya kukuhusu na ukayatumia kama ndio mwongozo wako.
Mawazo hasi ni kama magugu usipoyang'oa mizizi itaendelea kuchipua ndani yako na kukurudisha nyuma kila siku.
5.KUTOTHAMINI ULICHONACHO
Kama unashindwa kushukuru kile ulichonacho sasa basi huna haja ya kupata la ziada.
Kutothamini
ulichonacho sasa kutakufanya usione uzuri wa maisha uliyonayo sasa na
kujiangalia katika upande ule ambao umepungukiwa tu.
Inawezekana huna kila kitu ulichohitaji kuwa nacho kwa sasa lakini una kila kitu kitakachokuwezesha kusonga mbele.
Maisha yetu hayana ukamilifu lakini yana uzuri wake.
6.UNAITAFUTA FURAHA KUTOKA NJE
Utaalamu sio mkusanyiko wa maarifa; bali ni kujitambua kamili wewe ushakuwa nani.
Utajiri wa kweli hauhusiani na mali unazomiliki;
bali ni kusalimu amri kwa mahitaji yasiyo na mwisho.
Unachotafuta hakipo mahali kwingine
wala muda mwingine,
unachotafuta kipo hapa, na si kwingine
bali ndani yako.
Jinsi unavyozidi kuitafuta nje ndivyo inazidi kujificha ndani zaidi.
7.UNATAFUTA URAHISI
Kuna
siku utakuja kukaa chini na kutafakari ndipo utagundua kuwa kila chenye
thamani ulichonacho sasa kulikuwa na changamoto kukipata.
Na hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa,
kwasababu changamoto kubwa zinamuandaa mtu wa kawaida na mafanikio makubwa asiyategemea akipambana mpaka mwisho.
Mapambano siku zote yana sababu yake kutokea;
inawezekana kwa ajili ya kukupa uzoefu au kukufundisha.
Njia ya mafanikio haiwi na urahisi hata kidogo.
DUNIA INATOA NAFASI KWA KILA MTU KUONYESHA UWEZO WAKE NA AKAFIKIA MAFANIKIO ANAYOYAHITAJI.
JINSI TUNAVYOIONA INAZUNGUKA NDIVYO TUNAHITAJIKA KWENDA NAYO SAMBAMBA NA SI KUBAKI NYUMA YENYEWE IKISONGA MBELE.
ANZA LEO KUEPUKA MAMBO YALIYOTAJWA KATIKA HATUA HIZO JUU KUANZA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO
Saturday, 2 November 2013
Siri thelathini (30) za mafanikio
Huyu ni mdau wetu ametutumia utafiti wake mdogo alio nasi tumeiweka hewani kwa ajili yako !!
SIRI
THELATHINI (30) ZA MAFANIKIO
- Utafiti inaonyesha kuwa watu waliofanikiwa walifuata kanuni fulani fulani za mafanikio ambazo mtu yayote akizifuata kwa ukamilifu atafanikiwa,kwa hiyo kama ukitaka mafanikio fuata kanuni hizi :-
- Uwe na lengo na uweke lengo kubwa.
- Uwe na picha mawazoni kila siku ya kitu unachotaka kakifanya.
- Uwa na nia na hamu hasa ya kufikia lengo lako.
- Fanya kitu kimoja kwa wakati,epuka tabia ya kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.
- Kupata elimu au maarifa juu ya kazi au shughuli unayotaka kufanya,fahamu kuwa elimu tu bila kupata kanuni nyingine huwezi kufanikiwa.
- Kamwe usitake utajiri wa haraka kwa njia ya udanganyifu,fanya kazi.
- Usiwe mwepesi wa kukata tamaa unapokutana na matatizo au kuchelewa kutimiza lengo lako.
- Uwe na imani kuwa utafikia lengo lako na uzungumze mambo ya imani.
- Anzia mahali popote ulipo,anza na chochote ulichonacho usingoje mpaka upate hali nzuri ndipo uanze kujishughulisha ili kufikia lengo.
- Toa sadaka na zaka maradufu na Mungu atakubariki,jifunze kusaidia wenye shida na wanaohitaji msaada.
- Jifunze kusaidia wanaotaka kufanikiwa na wewe watakusaidia kufanikiwa,shinda wivu,usitake mafanikio kwa gharama ya mwingine.
- Usiwe unajilinganisha na wengine kiuwezo,tambua vipaji vyako na uvitumie.
- Uwe na tabia ya kujiamini kawa unaweza kufanya kitu unachotaka.
- Tumia mawazo yako kufanikisha jambo.
- Jenga tabia ya kujizuia,zuia misisimko iliyoko mwilini mwako kama vile hasira kufanya tendo la ndoa kabla ya wakati.
- Jihadhari sana na watu wanaokatisha tamaa na kamwe usiwaambie malengo yako.
- Jenga tabia ya kujiwekea akiba kwa ajili ya mipango yako ya baadae.
- Jifunze kutunza wakati na usitumie wakati kwa mambo yasiyofaa.
- Uwe mwangalifu na maneno unayotamka,kila mara tamka maneno yenye mafanikio.
- Kamwe usiogope kusemwa au kuchekwa wote waliofanikiwa walichekwa hivyo hivyo.
- Uwe tayari kulipa gharama ya mafanikio ili kutuimiza lengo.
- Sikiliza mashauri kwa watu unaowaamini na wanaokupenda.
- Jifunze kutokana na makosa au kosa la mtu mwingine
- Usiweke fedha kama kipaumbele katika lengo lako kuu.
- Jenga uhusiano na ushirikiano mzuri na watu,uwe na amani na watu wote,heshimu kila mtu,hakuna aliyefanikiwa bila msaada.
- Tunza mwili wako na mavazi yako uwe na muonekano mzuri,kumbuka kutunza afya yako
- Jikubali kama ulivyo kwa kufanya mambo ya namna yako.
- Shika amri za Mungu zote na dhambi ikome maishani mwako.
- Mfanye Mungu wa kwanza kwa kila jambo unalotaka kufanya naye atakusaidia kufikia malengo yako.
- Mwambie Mungu nini unataka na kwa nini unataka ila usiombe vitu vya ubinafsi.
Yamkini na wewe unayo makala ya kuwatia moyo watu wengine au za kuwafunza katika harakati hizi za maisha,basi usisite kutuma kupitia rajombo@hotmail.com nasi tutaiweka hewani bila hiyana !!.
Subscribe to:
Posts (Atom)