Friday, 22 November 2013

UMASKINI TANZANIA NI HALALI YETU KUWA NAO?

Mada yetu ya leo inatahusu juu ya umaskini wa nchi yetu Tanzania na maisha ya wananchi wake.Hivi ushawahi jiuliza kama umaskini wa nchi yetu Tanzania unatokana na nini na unasababishwa na kitu gani?Kwa haraka haraka umaskini ni ile hali ya kutoweza kujikizi kwa mahitaji ya vitu muhimu kama vile Malazi, chakula na maradhi.Kwahiyo ukiweza kumudu vitu hivyo ndio unaepukana na hali ya kuwa masikini lakini kwa nchi kiujumla ni kwamba masikini ni ile nchi ambayo wakazi wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku.Nchi nyingi za Africa zinaishi chini ya dola moja lakini zinakutana na mambo makubwa sana yanayowafanya waishi chini ya dola moja kama vile vita,njaa,ukame na tofauti za kisiasa zinazosababishwa na serikali tawala na vyama vya upinzani vinazotokea na kugombea madaraka na wengine kukataa kutoka madarakani hata kama wameshindwa uchaguzi na kung'ang'ania madarakani tu kwa nguvu.Vita katika Tanzania havijawahi kuwepo na wananchi wake wameishazoea kuishi kwa amani sana maana hawajui kabisa tofauti na nchi zingine lakini bado nchi ni maskini na watu wake ni maskini pia.Mfano wa nchi maskini zenye vita ni kama hivi katika picha hapa chini:
Hii picha inaonyesha jinsi ambavyo watu hawawezi kufanyakazi zao kwa hali ya amani kutokana na vita hivyo kwa hivyo wananchi wanakuwa na wasiwasi wa maisha yao badala ya kujiwekeza katika shughuli za kilimo au biashara ambazo zinaweza kuwapatia maisha yao ya kila siku.Lakini hali hii ni tofauti kabisa na huku kwetu Tanzania ambako watanzania tumekuwa maskini tu wakati nchi iko shwari na ina neema ya mvua katika sehemu kubwa sana ya Tanzania mfano katika mikoa mingi mvua ipo tu na tena ya kutosha mpaka huwa ina sababisha mafuriko.Hebu angalia baadhi ya maeneno mazuri yenye rutuba na mvua ya kutosha Tanzania katika picha hiz hapa:


Je ni kweli tuendelee kuilaumu serikali yetu inayoshindwa kutumia rasilimali za nchi yetu kwa maendeleo ya wananchi na kuendelea kuwafaidisha wawekezaji wa kigeni na baadhi ya wananosaini mikataba ya kiraghai?Mimi nafikiri tujikwamuwe wenyewe tu kwakwenda kuwekeza katika maeneo kama haya ingawa mwanzo mgumu tuanze hata kwa hilo jembe la mkono baadae tuna weza kujikwamuwa kwa kununua vifaa vingine tukiwa na fedha ya kutosha kwani hata ukuta wa beijing ulijengwa kwa mikono ya wananchi wa china bila mashine na wakaweza.Cha msingi ni kujipanga tu na tukaweza kujikwamua katika hali tuliyonayo badala kuendelea kulaumu serikali isiyokuwa na masikio ya kusikia wananchi wake.Kulima hakuitaji mtaji mkubwa wala ufugaji wa kuku wakienyeji hauhitaji mtaji mkubwa zaidi ya kuwa na uvumilivu tu katika hilo na baadae tuishi katika maisha mazuri na kuikwamua nchi yetu wenyewe na sio kutegemea wanasiasa walaghai wanaojinufaisha wenyewe tu.

No comments:

Post a Comment