Huyu ni mdau wetu ametutumia utafiti wake mdogo alio nasi tumeiweka hewani kwa ajili yako !!
SIRI
THELATHINI (30) ZA MAFANIKIO
- Utafiti inaonyesha kuwa watu waliofanikiwa walifuata kanuni fulani fulani za mafanikio ambazo mtu yayote akizifuata kwa ukamilifu atafanikiwa,kwa hiyo kama ukitaka mafanikio fuata kanuni hizi :-
- Uwe na lengo na uweke lengo kubwa.
- Uwe na picha mawazoni kila siku ya kitu unachotaka kakifanya.
- Uwa na nia na hamu hasa ya kufikia lengo lako.
- Fanya kitu kimoja kwa wakati,epuka tabia ya kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.
- Kupata elimu au maarifa juu ya kazi au shughuli unayotaka kufanya,fahamu kuwa elimu tu bila kupata kanuni nyingine huwezi kufanikiwa.
- Kamwe usitake utajiri wa haraka kwa njia ya udanganyifu,fanya kazi.
- Usiwe mwepesi wa kukata tamaa unapokutana na matatizo au kuchelewa kutimiza lengo lako.
- Uwe na imani kuwa utafikia lengo lako na uzungumze mambo ya imani.
- Anzia mahali popote ulipo,anza na chochote ulichonacho usingoje mpaka upate hali nzuri ndipo uanze kujishughulisha ili kufikia lengo.
- Toa sadaka na zaka maradufu na Mungu atakubariki,jifunze kusaidia wenye shida na wanaohitaji msaada.
- Jifunze kusaidia wanaotaka kufanikiwa na wewe watakusaidia kufanikiwa,shinda wivu,usitake mafanikio kwa gharama ya mwingine.
- Usiwe unajilinganisha na wengine kiuwezo,tambua vipaji vyako na uvitumie.
- Uwe na tabia ya kujiamini kawa unaweza kufanya kitu unachotaka.
- Tumia mawazo yako kufanikisha jambo.
- Jenga tabia ya kujizuia,zuia misisimko iliyoko mwilini mwako kama vile hasira kufanya tendo la ndoa kabla ya wakati.
- Jihadhari sana na watu wanaokatisha tamaa na kamwe usiwaambie malengo yako.
- Jenga tabia ya kujiwekea akiba kwa ajili ya mipango yako ya baadae.
- Jifunze kutunza wakati na usitumie wakati kwa mambo yasiyofaa.
- Uwe mwangalifu na maneno unayotamka,kila mara tamka maneno yenye mafanikio.
- Kamwe usiogope kusemwa au kuchekwa wote waliofanikiwa walichekwa hivyo hivyo.
- Uwe tayari kulipa gharama ya mafanikio ili kutuimiza lengo.
- Sikiliza mashauri kwa watu unaowaamini na wanaokupenda.
- Jifunze kutokana na makosa au kosa la mtu mwingine
- Usiweke fedha kama kipaumbele katika lengo lako kuu.
- Jenga uhusiano na ushirikiano mzuri na watu,uwe na amani na watu wote,heshimu kila mtu,hakuna aliyefanikiwa bila msaada.
- Tunza mwili wako na mavazi yako uwe na muonekano mzuri,kumbuka kutunza afya yako
- Jikubali kama ulivyo kwa kufanya mambo ya namna yako.
- Shika amri za Mungu zote na dhambi ikome maishani mwako.
- Mfanye Mungu wa kwanza kwa kila jambo unalotaka kufanya naye atakusaidia kufikia malengo yako.
- Mwambie Mungu nini unataka na kwa nini unataka ila usiombe vitu vya ubinafsi.
Yamkini na wewe unayo makala ya kuwatia moyo watu wengine au za kuwafunza katika harakati hizi za maisha,basi usisite kutuma kupitia rajombo@hotmail.com nasi tutaiweka hewani bila hiyana !!.
No comments:
Post a Comment